“CRACK”/”UNLOCK” Modem ya 3G ya line Moja iweze kutumika line zote (Tigo,Voda,Airtel,Halotel ,n.k)

Kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia na watu wengi kutumia vifaa vingi vya kiteknolojia blog yetu imeamua kukuongezea kipengele ambacho kitakuwa kikihusu ushauri, utatuzi na elimu kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusiana na teknolojia na leo tunajifunza jinsi unavyoweza kufungua modem ya 3G inayotumia mtandao mmoja ikatumika katika mitandao yote
Hii ni kwa faida yako na bila Malipo yeyote, Kama una modem ambayo inaruhusu kutumia Mtandao moja tu, na unashindwa jinsi ya kufanya ili kutumia mitandao mingine, wengine hujikuta wananunua modem ya kila mtandao. Najua kuna baadhi wanafahamu jinsi ya kufanya ila wengi wao hawajui. Nipo kwa ajiri ya kuwaelekeza wale ambao hawajui jinsi ya kufanya modem hiyo inayotumia mtandao mmoja kutumia mitandao yote. Mfano modem yako ulikuwa unaitumia mtandao wa Vodacom tu, Sasa utaweza kutumia na mitandao mingine kama Tigo, Airtel, Halotel, n.k


Image result for modem 3g

Awali ya yote, Unahitaji: 

1. Kompyuta binafsi

2. Modem

3. Huawei Unlocker Application

4. Na IMEI za Modem yako (Itaelezewa hapo chini)
HATUA ZA KUFANYA 


1. Ingiza Modem yako kwenye Kompyuta

2. Install Modem kwenye Kompyuta

3. Kisha uchomoe kwenye kompyuta

4. Iweke Aina nyingine ya mtandao “line” kama Modem ni ya Airtel weka line nyingine Mfano Tigo

5. Itakuomba UNLOCK CODE

6. Fungua Folder la Huawei Unlocker

7. Run the Huawei Unlocker Application

8. Ingiza IMEI code

9. Kisha bofya Calc,

10. Code iliyojitokeza ni code ambayo inayohitajika kwenye Modem yako

11. Bingooooooooo, Modem yako sasa imeshakuwa UNIVERSAL, Unaweza ukatumia line yeyote

Bonyeza hapo chini ili Kupakua Huawei Unlocker Application 

“CRACK”/”UNLOCK” Modem ya 3G ya line Moja iweze kutumika line zote (Tigo,Voda,Airtel,Halotel ,n.k) “CRACK”/”UNLOCK” Modem ya 3G ya line Moja iweze kutumika line zote (Tigo,Voda,Airtel,Halotel ,n.k) Reviewed by Admin on April 01, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.