VIDEO ZINAZOTAMBA MTANDAONI

  • Whispered_Band_Wapi_Mama Official Music Video
  • Mbosso - Nimekuzoea (Official Video)
  • Baadhi ya wabunge wazungumzia hoja binafsi ya Bashe
  • Hamza Kalala- Tufurahi na mwaka Mpya
  • Papii Kocha - Waambie (Official Video)
  • Mch: Daniel Timothy Jibu Lipo

HABARI ZA HIVI PUNDE NDANI YA LAELA YETU BLOG

Friday, 16 March 2018

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim waliwasili kituo Kikuu cha polisi Dar es salaam hadi wanatoka kituoni hawajahojiwa chochote.
Wakili Alex Masaba akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya Mwenyekiti huyo kuripoti amesema kuwa “Haiwezekani mtu anafika polisi anakaa tu kwenye makochi ya central anaambiwa aripoti tena.“
Viongozi hao wametakiwa kuripoti tena Alhamisi ya tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka huu.
Waliotakiwa kuripoti Polisi ni pamoja na Katibu Mkuu Chadema, Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika

Mh. Mbowe, Salum Mwalimu watoka polisi bila kuhojiwa chochote

By: Admin on: March 16, 2018
Leo March 16, 2018 Nakusogezea Exclusive Interview na Mwalimu kutoka shule ya Msingi Ngundusi iliyopo wilaya ya Ngara Kagera, amemzungumia mtoto Anthony Petro anayesoma Darasa la kwanza ambaye siku kadhaa alionekana kwenye mitandao ya kijamii akizungumza kumpeleka Baba yake mzazi kituo cha Polisi baada ya kusikia anauza sehemu eneo la nyumbani kwao.
“Kijana Antony ni mwanafunzi wangu wa darasa la kwanza na katika familia yao wapo watatu na wote ni wanafunzi wangu, maudhurio yake ni ya wastani, akikosa chakula uwa anaenda mjini kuomba msaada” -Mwalimu wa Anthony

Mwalimu wa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polisi kwa kuuza shamba, kaongea

By: Admin on: March 16, 2018
Tokeo la picha la barabara ya mwendokasi
Baada ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dart) kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, baadhi ya magari madogo, daladala na bodaboda wametumia fursa hiyo kupitisha magari yao katika barabara zinazotumika na magari hayo.
Mwananchi limeshuhudia daladala zikipita katika vituo hivyo huku zikishusha na kupakiza abiria katika kila kituo cha mwendokasi, huku trafiki wakielekeza baadhi ya magari kutoka kwenye barabara hizo.
Hata hivyo vituo vingi vya mwendokasi vimefungwa isipokuwa kituo cha Ubungo ambacho wahudumu wameonekana wamelala huku kukiwa hakuna abiria wanaoingia katika kituo hicho.
Dereva wa daladala linalofanya safari zake Mbagala Rangitatu – Simu 2000 Jafari Himid amesema kutokana na foleni iliyopo katika barabara hiyo, wameamua kutumia barabara za mwendokasi ili kuokoa muda.
“Bila kufanya hivi hatuwezi kuwahisha abiria na hizi barabara leo hazina matumizi, hata trafiki wanatuachia hawajatukamata,” amesema Jafari.
Hata hivyo barabara ya Morogoro Road ina foleni kubwa inayosababishwa na kipande cha barabara ya jangwani kujaa tope.

Baada ya Magari ya Mwendokasi Kusitisha Huduma ya Usafiri Daladala, Bodaboda Zatumia Njia ya Mwendokasi

By: Admin on: March 16, 2018Droo ya upangaji wa timu zitakazokutana kwenye hatua ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya tayari imeshafanyika.

Jumla ya timu 8 zilizokuwa zimefuzu kuingia hatua hiyo tayari kila mmoja ameshapangiwa mwenzake.

Mpangilio huo umekamilika kwa namna hii

Liverpool FC vs Machester City
Barcelona vs AS Roma
Juventus vs Real Madrid
Sevilla vs Bayern Munich

Mechi za mwanzo zitachezwa Aprili 3 mpaka 4 na zitarudiana wiki itakayofuata, Aprili

Droo ya Robo Fainali UEFA yakamilika: Liverpool kukutana na man City

By: Admin on: March 16, 2018

Tuesday, 13 March 2018

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa orodha ya majina ya Wabunge mbalimbali ambao wameteuliwa katika kamati mbalimbali za kudumu za Bunge ambao wataongoza kwa kipindi cha mwaka 2018-2020.

Wabunge mbalimbali wameteuliwa kuongoza kamati hizo za kudumu kwa kipindi hiko cha mwaka ambapo baadhi ya wabunge walioteuliwa ni  Mhe. Nnape Nnauye, Mhe. Andrew J. Chenge, Mhe. Emmanuel Mwakasaka na wengine.

Kufahamu wabunge hao na kamati zao angalia chati iliyopo hapa chini ikibainisha majina ya wenyekiti na makamu wao.

Orodha ya wenyekiti na makamu wenyekiti kamati ya kudumu ya bunge 2018-2020

By: Admin on: March 13, 2018
Viongozi wa Chadema waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi leo Jumanne Machi 13, 2018 wametakiwa kufika tena kituoni hapo Machi 16, 2018.

Licha ya kutakiwa kuripoti viongozi saba, waliofanikiwa kufika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.

Viongozi wengine watano akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshindwa kuripoti kutokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vilivyoanza leo mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, wametakiwa kuripoti Machi 16, saa 2:00 asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho Dk Mashinji amesema, “Viongozi wote wameshatoa maelezo yao. Leo tumeripoti wawili na viongozi wengine ni wabunge na wapo Dodoma walishindwa kujigawa katika mambo mawili.”

Viongozi CHADEMA waripoti tena kituo cha Polisi

By: Admin on: March 13, 2018
Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu na wenzake jana ulidai mahakamani kuwa umefunga ushahidi dhidi ya mashtaka kutumia na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kwa msanii huyo.

Madai hayo yalitolewa jana na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza ushahidi wa shahidi wa nne na wa tano mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Awali, shahidi wa nne, mjumbe wa nyumba 10, Steven Ndonde alidai mahakamani hapo kuwa siku ya tukio aliitwa kushuhudia upekuzi nyumbani kwa Sepetu.

Alidai kuwa wakati upekuzi unaendelea walikuta kipisi cha msokoto katika chumba cha nguo na viatu cha msanii huyo na chumba cha mfanyakazi wake walikuta kipisi kingine.

Hata hivyo, shahidi huyo alipohojiwa na wakili wa utetezi Albart Msando alikana kuwakuta washtakiwa wote wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika upekuzi huo.

Shahidi wa tano, Koplo wa Polisi Robert (31), alidai kuwa Februari 4, 2017 alipokea maagizo kutoka kwa bosi wake ya kupeleka vielelezo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwamo msokoto mmoja na vipisi viwili vya dawa za kulevya idhaniwayo kuwa bangi.

"Nilipeleka, vilipokelewa ofisi ya mkemia mkuu, baada ya kupokelewa niliandika barua kuhusu vielelezo hivyo," alidai Koplo Robert.

Kakula alidai baada ya kuita mashahidi watato dhidi ya washtakiwa upande wa Jamhuri imefunga kesi yao.

"Mheshimiwa hakimu tunaiachia mahakama iamue sisi upande wa Jamhuri tumefunga kesi yetu..." Alidai Kakula.

Wakili Msando aliomba upande wa utetezi kuwasilisha hoja za kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la ndani ya siku 10.

Upande wa Jamhuri ulidai utawasilisha majibu Aprili 3, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Mbali na Sepetu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Ilidaiwa kuwa Februari mosi, mwaka jana katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, Sepetu alitumia dawa za kulevya aina ya bangi. Washtakiwa walikana mashitaka.

Upande Wa Mashtaka Wafunga Ushaidi Kesi Ya Wema Sepetu

By: Admin on: March 13, 2018
Mwanamuziki wa Bongo fleva Anayezidi kufanya vizuri hivi sasa Aslay amefunguka na kusema hana Uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii mwenzake Nandy.

Kumekuwa na maneno mengi mengi ambayo yamekuwa yakisababishwa na ukaribu uliopo kati ya Nandy na Aslay ambapo mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii imesemakana kuwa wawili hao ni wapenzi.

Kwenye Interview aliyofanya Friday Night Live ya East Africa Tv, Aslay amefunguka na kusema ukaribu aliokuwa nao na Nandy ni wa kikazi tu sio zaidi ya hapo na amesisitiza kuwa yeye tayari ana mpenzi wake na familia.

" Nafikiri watu wanaonifatilia watakuwa wanajua kuwa mimi nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy nipo naye kwenye kazi zetu za kimuziki tunazofanya hakuna kingine cha zaidi kinachoendelea kati yangu na Nandy”.

Nandy na Aslay wanakimbiza na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao umefikisha zaidi ya viewers milioni tatu YouTube kwa mwezi mmoja lakini pia wameshawahi kufanya ngoma nyingine iliyofanya vizuri siku za nyuma iliyoitwa Mahabuba.

Aslay Akiri hana mahusiano na Nandy

By: Admin on: March 13, 2018

Tokeo la picha la tshishimbi yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limemtangaza Mchezaji, Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Februari.

Tshishimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kuvuna alama 12 huku akifunga mabao matatu na akitengeneza moja.

Mechi ambazo Tshishimbi alihusika kwenye ushindi katika mwezi Februari ni dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda na Lipuli ya Iringa.

Pius Buswita (Young African) na Emmanuel Okwi (Simba SC) ni wachezaji ambao waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo kwa mwezi huu wa pili.

Tshishimbi ambaye ni mshindi wa tuzo hii, atazawadiwa kitita cha milioni moja sambamba na king'amuzi cha Azam TV.

Tshishimbi atangazwa mchezaji Bora Ligi kuu ya Vodacom Mwezi Februari

By: Admin on: March 13, 2018

Saturday, 10 March 2018Stories zilizo-trend kwenye mitandao ya kijamii ambapo msanii wa Bongo Fleva Dogo Janja amewaacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kupost picha iliyoacha comments nyingi kwenye ukurasa wake wa instagram.

Dogo Janja amepost cover ya wimbo wake mpya wa Wayu Wayu ambapo ameonekana kuvaa mavazi ya kisichana pamoja na viatu vya kike na pia kupaka lipstick kwenye cover hiyo kitu ambacho ni cha kushangaza kwa jamii za Kiafrika kwa mwanaume kuvaa mavazi ya msichana .

Muonekano huu wa Dogo Janja ambao umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ni record ambayo ameiweka katika tasnia ya muziki nchini ambapo hakuna msanii wa kiume ambaye amewahi kufanya kitu kama hicho.Dogo Janja Avaa Gauni na Kupaka Lipstiki Kwenye Wimbo wake, Mashabiki wake Wamtolea Mapovu

By: Admin on: March 10, 2018
Rais Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa hatobadilika na ataendelea kuwa yule yule katika kuwatumikia wananchi.

Pia amesema serikali itamega maeneo ya ardhi ya hifadhi na kuwapa wananchi ili yatumike katika shughuli za maendeleo.

Ametoa msimamo huo leo alipokuwa akifungua matumizi ya barabara ya Uyovu- Bwanga km 45 katika eneo la uyovu runzewe wilayani  Bukombe mkoani Geita.

“Sitobadilika kamwe mimi ni yule yule nitaendelea kuwatumikia watanzania wote,’’ amesema Magufuli

Kuhusu ardhi amesema hatua ya kumega ardhi ya hifadhi ni kufuatia kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watanzania tangu  nchi kupata uhuru.

“Ni ukweli usiopingika ni lazima maeneo ya hifadhi yamegwe na kupewa wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo hii ni kutokana na kwamba idadi ya watanzania imeongeza maradufu tangu nchi ipate  uhuru,’’ amesema Magufuli

Amewata wananchi kuwa na subra na kwamba serikali ipo katika mchakato wa kutoa maeneo hayo.

Rais amesema kutokana na ongezeko la watu maeneo ya kulima na ufugaji yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Akitolea mfano amesema kwa sasa matumizi ya ardhi kwa wilaya ya Bukombe ni asilimia 40 na asilimia 60 ni hifadhi.

“Hakuna sababu ya kuandamana wala kupigana kugombea ardhi, serikali itatoa ardhi,’’ alisisitiza.

Barabara hiyo ni kiunganishi cha mikoa ya Geita, Shinyanga, Kigoma, Kagera pamoja na nchi ya  Rwanda

Advertisement

Rais Magufuli: "Sitobadilika Hata Kidogo"...... Aahidi kumega Ardhi ya hifadhi kuwapa wananchi

By: Admin on: March 10, 2018

Thursday, 8 March 2018


Tokeo la picha la simba sc
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BODI ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya wenyeji Njombe Mji FC na Simba SC uliopangwa kufanyika Jumapili Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Hiyo inafuatia klabu ya Simba kuomba mchezo huo uahirishwe ili wapate fursa nzuri ya maandalizi kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry mjini Cairo wiki ijayo.
Simba inatarajiwa kumenyana na Al Masry Machi 17 mjini Cairo baada ya jana timu hizo kutoa sare ya 2-2 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Simba SC sasa hawatakwenda Njombe kucheza na Njombe Mji FC Jumapili ili wapate fursa ya kujiandaa vizuri na mechi dhidi ya Al Masry


Wakiwa wanahitaji ushindi wa 1-0 ugenini ili kusonga mbele, Simba SC wameonekana kuelekeza nguvu zao kwenye maandalizi mazuri ili watimize malengo yao.
Wakati huo huo; Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakiwakaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na kwamba Yanga nayo inakabiliwa na mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana Machi 17 tena baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza juzi, lakini hawahitaji kuahirishiwa mechi za Ligi Kuu ya hapa.
Yanga SC wao watatakiwa kushinda 2-0 ugenini wiki ijayo ili kuingia hatuan ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika – jambo ambalo ni gumu na kwa hali halisi ndani ya klabu hiyo wanaonekana kama wamekata tamaa.

Mechi ya SIMBA na Njombe mji yasogezwa mbele, kesho ni Yanga na Kagera Sugar

By: Admin on: March 08, 2018

 

Idadi ya Watembeleaji Wetu

TANGAZA NASI UYAONE MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO

Copyright © LAELA YETU BLOG | IMETENGENEZWA NA LAELA YETU BLOG TEAM |